1 Julai 2015 - 21:48
Machafuko ya uchaguzi yazuka Bujumbura Burundi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu sita wameuwawa akiwemo polisi mmoja katika mapambano ya ufyetulianaji risasi hii leo huko Bujumbura.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu sita wameuwawa akiwemo polisi mmoja katika mapambano ya ufyetulianaji risasi hii leo huko Bujumbura. Hilo ni tukio la kwanza la hivi karibuni kabisa nchini humo wakati wananchi wake wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa bunge uliosusiwa na upinzani na kushutumiwa na jumuiya ya Kimataifa. Mapigano yalizuka kwenye wilaya ya Cibitoke iliyoko kwenye mji mkuu wa Bujumbura ambako ni ngome ya upinzani  na ambako ni kitovu cha maandamano dhidi ya hatua ya rais Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais unaokuja.Zaidi ya watu 70 wameuwawa katika kipindi cha miezi miwili ya maandamano pamoja na jaribio la mapinduzi lililoshindwa lililosababishwa na ukaidi  wa rais Nkurunziza.Kuna Warundi kiasi 144,000 waliokimbilia katika nchi jirani.Watano kati ya watu sita waliouwawa leo wilani Cibitoke ni wanachama wa kundi lenye silaha kwa mujibu wa polisi .Aidha polisi imeema imezikamata silaha,ikiwemo bunduki na maguruneti.

Mwisho wa habari /291